Uelewa kabla ya mauzo
Tunaanza na gari, aina ya repair na finish unayotaka.
Kuhusu Sikkens Mawere
Sikkens Mawere Car Paints & Accessories Ltd. ni wauzaji, watumiaji na wasambazaji wa rangi za magari na vifaa vyake kwa wateja Tanzania.

Tulipo
Tupo Mwenge, Dar es Salaam, tukihudumia wamiliki wa magari, mafundi wa rangi, body shops, gereji na wanunuzi wa biashara. Tunauza bidhaa za Sikkens kutoka AkzoNobel pamoja na bidhaa na vifaa vinavyosaidia kazi nzima ya refinishing.
Tunafahamu kuwa rangi si kopo moja. Matokeo yanategemea maandalizi, bidhaa zinazoendana, mazingira ya kazi na ufundi wa anayepaka. Ndiyo sababu mazungumzo yetu ya mauzo huanza na kuelewa kazi.
Tunachoamini
Tunataka kila mteja ajue anachonunua, kwa nini anakihitaji na hatua gani itafuata.
Tunaanza na gari, aina ya repair na finish unayotaka.
Tunasisitiza bidhaa zinazofanya kazi pamoja, si majina ya bidhaa pekee.
Delivery bure Dar es Salaam na delivery inayopangwa Tanzania nzima.
Tunatumia uelewa wa bidhaa katika huduma halisi za upakaji wa magari.

Bidhaa tunazouza
Catalogue yetu inajumuisha mifumo ya rangi, primers, fillers, hardeners, reducers, clearcoats na vifaa vya maandalizi na polishing. Upatikanaji hutofautiana; thibitisha stock na timu yetu.
Angalia bidhaa→